• Kabudi
  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma (kulia) akimkabidhi vitabu vya Mpango Mkakati wa Miaka 5 wa Mahakama ya Tanzania (2015 - 2020) Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.. Palamagamba Kabudi alipomtembelea ofisini kwake leo (14/7/2017).
 • kabud
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof Palamagamba Kabudi (aliyesimama) akiongea na viongozi mbalimbali wa Mahakama alipotembelea Mahakama ya Tanzania leo (14/7/2017).
 • las
  Mwenyekiti wa iliyokuwa Sekretarieti ya Huduma ya Msaada wa Kisheria (LAS) Bi Theodosia Muhulo (kushoto) akikabidhi ripoti ya utendaji wa LAS kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bi. Edith Simtengu kuashiria kuanza kutumika kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria kwa Umma.
 • Makabidhiano ofisi
  Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison
  Mwakyembe (kulia) akimkabidhi Taarifa Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
  Palamagamba Kabudi katika makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Makao
  Makuu ya Wizara yaliyoko Chuo Kikuu cha Dodoma mjini Dodoma.
 • Makabidhiano ofisii
  Waziri Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi
  (katikati) akionyesha taarifa ya makabidhiano aliyopewa na Waziri wa
  Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe mara baada
  ya kukabidhiwa kushoto kwa Prof Kabudi ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon
  Mpanju ambaye alihudhuria makabidhiano hayo.
 • kadi
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
 • Waziri Kabudi awasili Dodoma
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.
 • Kabudi
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
 • balozi korea
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young alipomtembelea ofisini kwake mapema leo (17/11/2016) jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Msaidizi wa Balozi Bw. Song Wong (kulia) na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdala Kirumbu (kushoto).
 • felistas
  Mtanzania Felistas Joseph, amechaguliwa kuongoza Kamati ya nchi za Maziwa Makuu ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari (International Conference on Great Lakes Region –ICGLR).
 • koreaa
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiwaonesha Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young na Msaidizi wake Bw. Song Wong ramani ya Mkoa wa Mbeya na kuwakaribisha kutembelea vivutio vya Mkoa huo ikiwemo Ziwa Nyasa.
 • upr
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
 • uprr
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango (kulia) alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba Bw. Stanley Kamana.
 • Balozi Jaap
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akibadilishana mawazo na Balozi wa Uholanzi Bw. Jaap Fredericks kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria ofisini kwake leo tar.20/09/2016.
 • Balozi Korea
  Katibu Mkuu Pro. Sifuni Mchome wa Wizara ya Katiba na Sheria akiongea na Balozi wa Korea nchini Tanzania kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya Sheria.
 • Mwakyembe
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe atembelewa na Jaji Mkuu wa Australia Kusini Bw. Christopher Kourakis ofisini kwake jijini Dar es salaam.
 • Balozi Christopher
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika ya pamoja na Balozi wa Australia Kusini (wa pili kulia)baada ya mazungumzo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar es Salaam.
 • Balozi Christopher
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika ya pamoja na Balozi wa Australia Kusini (wa pili kulia)baada ya mazungumzo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar es Salaam.
 • Mwakyembe
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara athari za suala la ushoga na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.
 • Mwakyembe
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma katika ukumbi wa mikutano wa Wizara moja ya nyaraka ambazo zinatumiwa na asasi za kiraia zinazojihusisha na masuala ya ushoga nchini.

Habari Mpya

Viongozi

Upo Hapa: Home

Wizara ya Katiba na Sheria ilianzishwa kwa tamko la Rais toleo Na.20 la mwaka 2008. Wizara hii ndiyo mhimili Mkuu wa Serikali katika masuala yote ya Kisheria katika nchi. Jukumu la msingi la Wizara ni kuhakikisha kuwa kuna utawala wa Sheria unaozingatia Katiba ya nchi.

Aidha, ni jukumu la Wizara, kuona kwamba Serikali na Taasisi zake zinasimamia Sheria kwa ufanisi na kwa dhati na kuwa wananchi wanapaswa kufuata na kuheshimu Sheria. Kwa ujumla Wizara inalo jukumu la kuhakikisha  kunakuwepo mfumo wa Sheria unaotoa fursa sawa kwa watu wote katika jamii ili kuweza kuendesha shughuli zao kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.

 

dira
dhamira
dira
dhamira

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

 • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
 • Barabara ya Mkalama,
 • Jengo la Taaluma Na. 1,
 • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
 • S.L.B. 315,
 • DODOMA.
 • Simu:+255 26 2321680
 • Nukushi: +255 26 2321679
 • Tovuti www.sheria.go.tz
 • Barua pepe: km@sheria.go.tz