Wizara ya Katiba na Sheria ilianzishwa kwa tamko la Rais toleo Na.20 la mwaka 2008. Wizara hii ndiyo mhimili Mkuu wa Serikali katika masuala yote ya Kisheria katika nchi. Jukumu la msingi la Wizara ni kuhakikisha kuwa kuna utawala wa Sheria unaozingatia Katiba ya nchi.
Aidha, ni jukumu la Wizara, kuona kwamba Serikali na Taasisi zake zinasimamia Sheria kwa ufanisi na kwa dhati na kuwa wananchi wanapaswa kufuata na kuheshimu Sheria. Kwa ujumla Wizara inalo jukumu la kuhakikisha kunakuwepo mfumo wa Sheria unaotoa fursa sawa kwa watu wote katika jamii ili kuweza kuendesha shughuli zao kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.


