• wizaran6
    Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Fanuel Mbonde wakati akifungua kwa hotuba mafunzo ya ukimwi yaliyofanyika tarehe 20 machi,2013 katika ukumbi wa wizara.
  • wizaran4
    Mfanyakazi wa Wizara ya kattiba na Sheria Bw Robert Mtakasimba akipimwa afya yake na mshauri nasaha wa Ukimwi toka WAMATA Bw. Saleh S. Kadope baada ya mafunzo ya Ukimwi yaliyofanyika leo tarehe 20 Machi 2013 ukumbi wa wizara jijini Dar es salaam.
  • wizaran5
    Mfanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi,Florantina Fissoo akipimwa afya yake na mshauri nasaha wa Ukimwi toka WAMATA Bw. Saleh S. Kadope baada ya mafunzo ya Ukimwi yaliyofanyika leo tarehe 20 Machi 2013 ukumbi wa wizara jijini Dar es salaam.
  • wizaran7
    Mkurugenzi wa Utawala wa Rasilimali watu Bw.Moses Chitama akichangia mada wakati wa mafunzo ya ukimwi yaliyofanyika leo(20 Machi,2013) katika ukumbi wa Wizara jijini Dar es salaam.
  • naibu4
    Mh. Angellah Jasmini Kairuki Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akizindua Kijitabu cha “Mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza” katika Makao Makuu ya Ofisi za Tume za Haki za Binadamu mtaa wa Luthuli jijini Dar-es-salaam Machi 15, 2013. Aliyeshika kijitabu na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu Bi. Mary Massay. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Jaji Kiongozi Mstaafu Bw. Amiri Manento.
  • naibu5
    Mh. Angellah Jasmini Kairuki Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akionyesha Kijitabu cha “Mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza” baada ya uzinduzi wa kijitabu hicho katika Makao Makuu ya Ofisi za Tume za Haki za Binadamu mtaa wa Luthuli jijini Dar-es-salaam Machi 15, 2013. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu Bi. Mary Massay. Kushoto kwake ni Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw Julian Chandler.
  • naibu6
    Mh. Angellah Jasmini Kairuki Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa kijitabu cha “Mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza” baada ya uzinduzi wa kijitabu hicho katika Makao Makuu ya Ofisi za Tume za Haki za Binadamu mtaa wa Luthuli jijini Dar-es-salaam Machi 15, 2013. Kulia kwake ni Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Bi. Bernadetha Gambishi. Kushoto kwake ni Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw Bw Julian Chandler.
  • wizaran3
    Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Mathias Chikawe akiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuzindua basi la Wafanyakazi tarehe 4 Machi, 2013 katika jengo la Wizara jijini Dar es Salaam.
  • waziritanga
    Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Mathias Chikawe akisoma risala wakati wa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort kuanzia tarehe 28 Feb - Mach 1, 2013 mjini Tanga
  • kmtanga
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Fanuel Mbonde akisoma risala wakati wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa Tanga Beach Resort kuanzia Feb 28 - Machi 1, 2013 mjini Tanga.
  • tanga
    Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa baraza la Wafanyakazi uliofanyika kuanzia tarehe 28 Feb - 1 Machi, 2013 mjini Tanga
  • tanga
    Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakifuatilia Taarifa ya Idara ya Utawala na Rasilimali Watu iliyokuwa ikisomwa na Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Moses Chitama ambaye hayupo pichani wakati wa Baraza la Wafanyakazi lililo fanyika mjini Tanga 28 Feb - 1 Machi, 2013.
  • Naibu Waziri
    Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Jasmine Kairuki(Mb) akiwasalimia Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
  • Law school
    Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Mathias Chikawe akipanda mti alipotembelea na kukagua majengo ya Chuo cha Uanasheria kwa vitendo (Law School). Waziri pia alipata fursa ya kuongea na wafanyakazi wa Chuo hicho.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki(Mb).
  • serena
    Picha ya pamoja ya Watumishi wa Taasisi zinazotekeza Progamu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria iliyopigwa Serena Hotel wakati Mkutano wa majadiliano wa Ripoti ya Masuala ya Jinsia katika Taasisi hizo jijini Dar es salaam.
  • naibutmk
    Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Angellah Jusmine Kairuki akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Sophia Mjuna wakati alipotembelea Ofisini kwake tarehe 5 Mach,2013
  • mama sonyi
    Mkurugenzi wa Sera na Mipango,Bi Christina Sonyi wa Wizara ya Katiba na Sheria akimsikiliza kwa makini mwezeshaji wa Chuo Kikuu Mzumbe Dk.Ernest Mwasalwiba(ambaye hayupo pichani) wakati akifundisha juu ya uandikaji wa viashiria vya hatari vya Wizara katika mkutano wa kuboresha kitabu cha viashiria vya hatari vya Wizara uliofanyika Machi 22-23,2013 katika ukumbi wa mikutano wa Kibaha Mkoani Pwani
  • wakufunzi
    Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bibi Leticia Nchwali wa Wizara ya Katiba na Sheria akibadilishana mawazo na wawezeshaji wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Bwana Aloyce Maziku(katikati) na Dk.Ernest Mwasalwiba(kulia) wakati wa mkutano wa siku mbili wa kuboresha Kitabu cha Viashiria vya hatari vya Wizara uliofanyika Machi 22-23,2013 katika Ukumbi wa mikutano Kibaha Mkoani Pwani.
  • wakufunzi
    Washiriki wa Mkutano wa Kazi wa Kuboresha Kitabu cha Viashiria vya Hatari vya Wizara wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa Mifumo ya kompyuta Bwana Pankras Uwoya(hayupo pichani) wa Wizara ya Katiba na Sheria wakati akichangia mada katika Mkutano huo uliofanyika Machi22-23,2013 Katika ukumbi wa Mkutano Kibaha Mkoani Pwani.

Habari Mpya

Viongozi

Upo Hapa: Home

Wizara ya Katiba na Sheria ilianzishwa kwa tamko la Rais toleo Na.20 la mwaka 2008. Wizara hii ndiyo mhimili Mkuu wa Serikali katika masuala yote ya Kisheria katika nchi. Jukumu la msingi la Wizara ni kuhakikisha kuwa kuna utawala wa Sheria unaozingatia Katiba ya nchi.

Aidha, ni jukumu la Wizara, kuona kwamba Serikali na Taasisi zake zinasimamia Sheria kwa ufanisi na kwa dhati na kuwa wananchi wanapaswa kufuata na kuheshimu Sheria. Kwa ujumla Wizara inalo jukumu la kuhakikisha  kunakuwepo mfumo wa Sheria unaotoa fursa sawa kwa watu wote katika jamii ili kuweza kuendesha shughuli zao kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.

 

dhamira
dira
dhamira
dira