Mradi wa Mfumo Endelevu wa Kupambana na Rushwa Tanzania - BSAAT
Mradi wa Mfumo Endelevu wa Kupambana na Rushwa Tanzania - BSAAT
Mradi wa Mfumo Endelevu wa Kupambana na Rushwa Tanzania - (BSAAT)
Mradi huu unalenga kujenga uwezo wa Taasisi za haki Jinai katika mapambano dhidi ya rushwa nchini. Matokeo ya awali ya mradi huu ni pamoja na kuondoa mianya ya rushwa katika Mifumo ya kitaasisi inayohusika na masuala ya Haki-Jinai na kuongeza wigo wa kushughulikia mashauri ya rushwa kubwa nchini. Matokeo ya kati ya mradi huu ni kuwa na mifumo thabiti ya kisheria na kisera kwa ajili ya kudhibiti na kupambana na vitendo vya rushwa nchini. Matokeo ya muda mrefu wa mradi huu ni kuchangia kuondoa umaskini kwa Watanzania.