Vigezo Na Masharti
Kanuni na Masharti yafuatayo yanasimamia matumizi yote ya Tovuti, tovuti za mifumo na huduma ndani ya tovuti hii na taarifa na data zote za mifumo na huduma za Wizara ya Katiba na Sheria (MoCLA).
Huduma zetu zinatolewa kwa sharti la kukubalika kila marekebisho ya kanuni na masharti yaliyomo na kanuni nyingine za uendeshaji, sera, notisi na taratibu zitakazochapishwa na MoCLA kila baada ya muda.
Tambua kuwa tunaweza kuhuisha tovuti hii pamoja na huduma yetu na kanuni hizi zitatumika kwa uhuishaji wowote. Tafadhali soma makubaliano haya kwa makini kabla ya kutumia au kupata huduma zetu. Kwa kupata au kutumia sehemu yoyote ya huduma zetu, unakubali kufungwa na kanuni na masharti ya makubaliano haya. Iwapo hukubaliani na kanuni na masharti yote ya mkataba huu, hutaweza kupata au kutumia huduma yetu yoyote.
Marekebisho katika kanuni na masharti:
Kanuni na masharti yanaweza kubadilika wakati wowote bila ya taarifa. Nakala ya hivi karibuni ya kanuni na masharti ya Mamlaka itawekwa kwenye tovuti au zinaweza kuombwa wakati wowote kwa kuwasiliana na MoCLA.