Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Idara ya Utawala na Rasilimali watu

Idara ya Utawala na Rasilimali watu

Madhumuni

Idara ya Utawala na Rasilimali Watu ni mhimili wa Uendeshaji wa shughuli za Taasisi hii za kila siku. Katika kutekeleza wajibu wake Idara inamsaidia Mtendajji Mkuu wa Wizara ambaye ni Katibu Mkuu kuiongoza Wizara. Aidha, Idara hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa Taasisi ina nyenzo za kutosha za kufanyia kazi, nyenzo hizo ni pamoja na rasilimali watu, fedha, majengo, usafiri, samani, n.k. Idara ya Utawala na Rasilimali Watu pia inao wajibu wa kuwezesha Idara zingine “Line Departments” kutenda kazi zake. Pia ina jukumu la kusimamia utendaji kazi katika Taasisi kwa kuhakikisha kuwa malengo makuu ya Tasisi yanafikiwa

Idara ya Utawala na Raasilimali watu imegawanyhika katika sehemu kuuu mbili:-

Sehemu ya Utawala/Uendeshaji:

 1. Kuhakikisha watumishi wanafuata Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma;
 2. Kutafsiri Sheria na Kanuni za Utendaji kazi kwa watumishi katika eneo la kazi;
 3. Kuhakikisha Wizara ina vitendea kazi vya kutosha;
 4. Kusimamia utendaji wa Masjijala za Wizara;
 5. Kushughulikia masuala ya Itifaki;
 6. Kusimamia Usafiri, Ulinzi na Usalama wa Jengo;
 7. Kusimamia matengeneonzo ya vitemndea kazi vya Wizara, Majengo na bustani;
 8. Kusimamia ustawi wa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na Afya, Usalama, Michezo na Utamaduni;
 9. Kusimamia Maadili ya Utumishi wa Umma pamoja na kutoa elimu ya kuzuia na kupambana na Rushwa;
 10. Kusimamia masuala Mtambuka kama Jinsia, Ukimwi (HIV/AIDS) na kuwa mwakilishii wa masuala Mtambuka Wizarani;
 11. Kuratibu masuala ya Sekta binafsi katika Wizara;
 12. Kuratibu Utekelezaji wa Mikakati ya Kuboresha Utendaji Wizarani;
 13. Kushauri juu ya mbinu za kuongeza Ufanisi Wizarani;
 14. Kuratibu Utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja;

Sehemu ya Rasiliamali Watu:

 1. Kuratibu ajira, kuthibitisha kazini, kupandisha vyeo na uhamisho wa watumishi;
 2. Kuratibu na kuandaa Mpango wa Mafunzo wa watumishi wa Wizara;
 3. uandaa Mafunzo ya awali ya watumishi;
 4. Kuandaa Mpango wa Rasilimali Watu wa Wizara na mahitaji ya Wataalamu wa Wizara;
 5. Usimamizi na uendesheaji wa masuala ya Mishahara;
 6. Uratibu wa Mkakati wa Upimaji Utendaji Kazi ;
 7. Kushughulikia masuala ya likizo za wafanyakazi;
 8. Kushughulikia stahili mbalimbali za watumishi;
 9. Kushughulikia stahili za watumishi wanapostaafu kazi ama kuacha kazi