Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Kitengo cha Msaada wa Kisheria

Malengo:

kuratibu na kudhibiti utoaji wa huduma bora na kwa wakati wa msaada wa kisheria kwa watu wasiojiweza.

Kitengo hiki kitatekeleza shughuli zifuatazo:

  1. kuratibu na kudhibiti watoa msaada wa kisheria na utoaji wa huduma za msaada wa kisheria.
  2. kufuatilia na kumshauri Waziri juu ya umuhimu wa mfumo wa msaada wa kisheria wa kitaifa hasa juu ya utaratibu wa kulinda haki za kisheria za watu walio katika mazingira magumu.
  3. Kuratibu bima ya miongozo ya sera na taratibu za kawaida za uendeshaji wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wasiojiweza.
  4. kufuatilia na kutathmini utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wasiojiweza.
  5. kuamua malalamiko na migogoro kati ya umma na watoa msaada wa kisheria
  6. kusimamia utekelezaji wa mipango ya msaada wa kisheria kwa ufanisi na utendaji mzuri wa huduma ya msaada wa kisheria.
  7. kuhakikisha kwamba msaada wa kisheria unatumika kama chombo cha kuwezesha utatuzi mbadala wa migogoro
  8. kuwasiliana na kushiriki katika masuala ya kisheria yanayohusiana na ukatili dhidi ya wanawake na Watoto
  9. kuratibu na kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa itifaki ya ICGLR ya kuzuia mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na aina zote za ubaguzi.

Kitengo hiki kinaongozwa na Mkurugenzi ambaye pia ni Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria.