Mkurugenzi Msaidizi wa Sera, Tafiti na Ubunifu, Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Abel Sengasenga,akipokea maoni ya wadau kuhusu mchakato wa kuwa na sera jumuishi itakayoboresha mfumo wa haki jinai kwa maslahi ya Watanzania wote. Aprili 16, 2025 Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha ameipongeza Wizara kwa maono ya kuanzisha elimu ya Uraia na Katiba kwa Wanafunzi Vyuo Vikuu na katika ngazi za chini za elimu na amesema hatua hiyo ni muhimu kwani itawasaidia Watanzania kutambua tunu zao na kuziishi. Aprili 16, 2025.
Katibu Mkuu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi akizungumza na Ujumbe kutoka Chuu Kikuu Mzumbe (hawapo pichani) ukiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha Ofisi kwake Mtumba, jijini Dodoma. Aprili 16, 2025.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akipokea nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Bi. Jane Lyimo mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo yaliyolenga kufikia makubaliano na uandaaji wa maudhui ya elimu ya Katiba na Uraia kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu. Aprili 16, 2025.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi tarehe 16 Aprili, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Chuu Kikuu Mzumbe ukiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha ikiwa ni hatua za awali za kuwezesha kuingia makubaliano kati ya Wizara na Chuo Kikuu Mzumbe ili kuweza kuja na mbinu mbalimbali zitakazotumika katika kuhakikisha maudhui ya Elimu ya Urai na Katiba yanachopekwa katika Mitaala ya Vyuo na inawafikia Wanafunzi katika Vyuo Vikuu.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali ambapo amewapongeza kwa kuendelea kutoa Huduma za Kisheria kupitia kliniki mbalimbali za Kisheria. Aprili 15, 2025 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria na kupokea maelezo ya shughuli za Kisheria zinazofanywa na Wizara kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma Bi. Angela Anatory wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali uliofanyika tarehe 15 Aprili, 2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Kagera tarehe 14 Aprili, 2025
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Jasson Rwezimula akitoa Salaam za Wizara wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Kagera. Tarehe 14 Aprili, 2025.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na viongozi mbalimbali mara bada ya kuwasili katika Uwanja wa Uhuru (Mashujaa) Mkoani Kagera kwa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia leo Aprili 14, 2025.