Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Access to Justice for Sustainable Development in Tanzania

Mradi wa Access to Justice for Sustainable Development in Tanzania

Mradi huu umejikita katika kujenga uwezo wa Wizara katika kuwezesha mifumo ya kisera, kisheria na kiutawala katika upatikanaji wa haki kwa maendeleo endelevu ya Taifa. Matokeo ya awali ya mradi huu ni kuimarisha mifumo ya usimamizi wa haki nchini, uratibu wa shughuli za haki jinai, haki za binadamu na utawala bora, utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, uamgalizi wa utajiri na maliasilia za nchi, kushughulikia viashiria vya matukio ya kimbali nchni. Matokeo ya kati ya mradi huu ni upatikanaji wa haki nchini unawezesha maendeleo endelevu ya Taifa. Matokeo ya muda mrefu ni mifumo ya utoaji haki inawezesha wananchi kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.