Kitengo cha TEHAMA
Kitengo cha TEHAMA
Malengo:
Kutoa utaalamu wa huduma za matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mmawasiliano (TEHAMA) kwa Wizara.
Kitengo hiki kinatekeleza shughuli zifuatazo:
- Kutekeleza uendelezaji wa TEHAMA pamoja na Sera ya Serikali Mtandao;
- Kuandaa na kuratibu Maunganisho ya Teknolojia yaHabari na Mawasiliano Wizarani;
- Kuhakikisha Hardware na Software zinatunzwa vyema;
- Kuratibu na kutoa ushauri wa Kitaalam katika ununuzi wa Software na Hardware za Wizara;
- Kuanzisha na kuratibu matumizi ya mawasiliano ya Barua Pepe, Locala Area Network na Wide Area Network;
- Kubuni, kuendeleza, kusimika, kusimamia na kutunza miundombinu ya TEHAMA na mifumo ya habari na mawasiliano kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao;
- Kuandaa na kutekeleza mpango wa huduma endelevu kw aWizara;
- Kutoa ushauri wa kiufundi kuhusu mifumo na miundombinu ya TEHAMA ya Wizara;
- Kutoa huduma na usaidizi kwa watumiaji;
- Kuratibu uhifadhi wa data;
- Kutekeleza huduma za usalama za TEHAMA; na
- Kufanya tafiti na kupendekeza maeneo ya kutumia TEHAMA kama chombo cha kuboresha utoaji wa huduma kwa Wizara;
Kitengo kinaongozwa na Mkuu wa Kitengo