Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wakati Mhe. Waziri alipofika ofisini hapo kutoa salamu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bi. Bahati Geuzye akihutubia wakati akifungua kuanza kwa mafunzo ya Waratibu 100 wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid campaign) kutoka Halmashauri tisa za mkoa wa Mtwara, tarehe 23 Januari, 2025.
Timu ya Utangulizi ya Wizara ya Katiba na Sheria ikiongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Msambazi pamoja na timu ya Wataalamu wakiwa katika kikao cha awali cha kupitia utekelezaji wa shughuli mbalimbali zitakazofanyika wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Kigoma. Tarehe 22 Januari, 2025 Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Dkt. Rashidi Chuachua.
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiendelea na mazoezi ya viungo Januari 16, 2025 Mtumba Jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria katia Mikoa sita.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi katikati akiongoza mazoezi ya utimamu wa mwili kwa baadhi ya wajumbe wa Menejimenti na Watumishi wa Wizara hiyo Januari 16, 2025 Mtumba Jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika Mikoa Sita.
Waratibu wa Mawakili wa Serikali, Wahadhiri Wasaidizi wa Vyuo Vikuu na Mawakili wa Kujitegemea kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa Waratibu wa Mikoa na Halmashauri kuhusu utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku mbili katika Chuo cha Uongozi Mwl. Nyerere Kibaha, Pwani, tarehe 14 Januari, 2025.
Wizara ya Katiba na Sheria imetoa mafunzo kwa Waratibu wa Mikoa na Halmashauri kuhusu utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Mafunzo hayo yameanza tarehe 14 Januari, 2025 katika Chuo cha Uongozi Mwl. Nyerere Kibaha, Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi akipokea zawadi kutoka kwa Vijana watoa Msaada wa Kisheria waliojiunga na Wizara ya Katiba na Sheria miezi minne iliyopita kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Vijana hao wapatao 12 waliowakilishwa wameoneshwa kuguswa na utendaji kazi wa Katibu Mkuu na moyo wa kuwajali. Tarehe 10 Januari, 2025 Mtumba, Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Wizara Mtumba, jijini Dodoma tarehe 8 Januari, 2025 kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na ugeni kutoka Ubalozi wa Japan nchini Tanzania ukiongozwa na Mhe. Balozi Yasushi Misawa wakati alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma tarehe 8 Januari, 2025 kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.