Majukumu ya Wizara
Majukumu ya Wizara
- Kuweka Sera kwa ajili ya mambo ya kisheria na utekelezaji wake;
- Kushughulikia mambo ya Kikatiba;
- Kusimamia mfumo wa haki na utoaji haki;
- Kuandika Sheria;
- Kuendesha mashtaka ya jinai;
- Kuhakiki mikataba mbalimbali inayohusu Serikali,
- Kuendeshaji mashauri ya madai yanayohusu Serikali na uratibu wa sheria za kimataifa;
- Kushughulikia masuala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria;
- Kurekebisha sheria mbalimbali za nchi;
- Kushughulikia urejeshwaji wa wahalifu na ushirikiano wa mataifa kwenye makosa ya jinai;
- Kusajili matukio muhimu ya binadamu kama vizazi, vifo, ndoa, talaka, ufilisi nk;
- Kuboresha utendaji na maendeleo ya rasilimali watu iliyo chini ya Wizara;
- Kuratibu shughuli za taasisi, mipango na miradi chini ya Wizara.