Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Bi. Makondo afanya mazungumzo na Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani

Imewekwa: 18 Jul, 2023
Bi. Makondo afanya mazungumzo na Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akiwa na Menejimenti ya Wizara hiyo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Marekani nchini ulioongozwa na Balozi Michele Sison kwenye Ofisi za Wizara Mtumba Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2023.

Katika mazungumzo yao pande zote mbili zimepongeza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Marekani kwenye nyanja mbalimbali na kutaka ushirikiano huo uendelee pia kwenye sekta ya sheria kwa kuwajengea uwezo wa wataalamu wa ndani katika masuala ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, uandishi wa mikataba na kufanya tafiti kwenye uandishi wa mikataba ya kimataifa.

Aidha, Ujumbe huo umepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye maboresho ya sheria mbalimbali nchini kwa manufaa ya watanzania.