Dkt. Chana Awasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Kamati ya Bunge
Dkt. Chana Awasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Kamati ya Bunge
Imewekwa: 14 Aug, 2024
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Sura ya 425 (THE LAW SCHOOL ACT CAP 425) mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, katika ukumbi mdogo wa Bunge jijini Dodoma, Agosti 14, 2024.
Muswada huo unapendekeza kufanya Marekebisho katika Sheria husika kwa lengo la kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizobainika katika utekelezaji wa masharti ya Sheria.