Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yapokea Miswada ya marekebisho ya Sheria mbalimbali
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yapokea Miswada ya marekebisho ya Sheria mbalimbali
Imewekwa: 26 May, 2023

Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro, ameongoza Timu ya Wataalam wa Wizara ya Katiba na Shera, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Shirika la Reli, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kuwasilisha Miswada ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali kwa Mwaka 2023 na Urekebu wa Sheria wa Mwaka 2023 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria leo tarehe 26 Mei, 2023, Jijini Dodoma.