Maswi Afanya Mazungumzo na Mshauri Elekezi wa BSAAT
Maswi Afanya Mazungumzo na Mshauri Elekezi wa BSAAT
Imewekwa: 14 Aug, 2024
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi, 13 Agosti 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Mshauri Elekezi wa Programu ya Kujenga Uwezo wa Taasisi katika kupambana na rushwa (Building Sustainable Anti- Corruption Action in Tanzania - BSAAT).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma, taarifa ya utekelezaji wa programu hiyo iliwasilishwa na kujadili maeneo ya mashirikiano kati yao na Wizara katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai.