Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Mkutano wa 77 wa Haki za Binadamu na Watu kufanyika Jijini Arusha

Imewekwa: 28 Jun, 2023
Mkutano wa 77 wa Haki za Binadamu na Watu kufanyika Jijini Arusha

William Mabusi - WKS

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) ameongoza timu ya Wizara kwenye Kikao Kazi kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa 77 wa Haki za Binadamu na Watu utakaofanyika hapa nchini mnamo tarehe 20 Oktoba mpaka 9 Novemba, 2023 mkoani Arusha na kuagiza usimamizi mzuri wa maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo.

Kikao Kazi hicho kimefanyika Jijini Arusha tarehe 28 Juni, 2023 na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Makondo, Mwenyeji Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. John Mongella, ndugu Steven Zelothe  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha miongoni mwa wengine.

Akiongea katika Kikao Kazi hicho Bi. Makondo alielezea chimbuko la Mkutano huo na alisema ni heshima kwa nchi kuwa mwenyeji wa Mkutano huo akibainisha kuwa nchi itanufaika kijamii, kiuchumi, kidiplomasia na haki za binadamu.

Akitoa shukrani zake kwa Wizara, Mkuu wa Mkoa ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuchagua Mkoa wa Arusha kuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa unaoangazia masuala ya haki za binadamu na watu.