Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mwanza Yahimizwa Uwajibikaji
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mwanza Yahimizwa Uwajibikaji
Imewekwa: 19 Mar, 2025

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Machi 18, 2025 Jijini Mwanza ameongoza kikao na watumishi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Mkoa huo ambapo amewahimiza umuhimu wa uwajibikaji katika kazi zao.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Ndumbaro amesisitiza kwamba ni muhimu kwa watumishi hao kuongeza ufanisi ili kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi na kusaidia katika utoaji wa Haki kwa wananchi.
Nae Mkuu wa Mashtaka wa Mkoa huo Bw. Joseph Mahugo, amemthibitishia Waziri Ndumbaro kwamba ofisi yake itaendelea kutoa huduma bora kwa maslahi ya taifa.
Ziara ya Waziri Ndumbaro Jijini Mwanza ina lengo la kufanya ukaguzi wa shughuli za ofisi hiyo na kuona jinsi wanavyoweza kuboresha huduma zao kwa umma.