Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

TARIFA KWA UMMA

08 Dec, 2025

Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Msajili wa Watoa huduma za Msaada wa Kisheria inapenda kuwakumbusha watoa Huduma za Msaada wa Kisheria na wadau  wa Msaada wa Kisheria wote kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Msaada wa Kisheria, Sura ya 21 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2018 ni marufuku kwa mtu au taasisi yoyote kutoa Huduma za Msaada wa Kisheria bila kuwa imesajiliwa na Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria.