Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Salva Kiir Mayardit Awasili Nchini na Kulakiwa na Dkt. Chana

Imewekwa: 23 Nov, 2023
Salva Kiir Mayardit Awasili Nchini na Kulakiwa na Dkt. Chana

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit amewasili nchini tarehe 23/11/2023 na kupokewa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kushiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha.

Mara ya mwisho Rais Salva Kiir kuja nchini ilikuwa April 15, 2016 ambapo alikutana na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya utiaji saini wa Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo unahudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Uganda, Rwanda, na Sudan Kusini.