Tathmini ya Ukarabati Jengo La Usuluhishi Ikamilike Kwa Wakati
Tathmini ya Ukarabati Jengo La Usuluhishi Ikamilike Kwa Wakati
Imewekwa: 07 Jul, 2024

Hyasinta Kissima – WKS Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini Julai 6, 2024 akiwa ameambatana na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wametembelea katika jengo linalotarajiwa kutumika kuwa Kituo cha Usuluhishi kilichopo Temeke, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Sagini ameelekeza kuharakishwa kwa kazi ya kufanyika kwa tathmini ya ukarabati wa jengo hilo inayofanywa na TBA ili ukarabati ukamilike kwa wakati na jengo hilo lianze kutumika.
Aidha, Mhe. Sagini ameelekeza Sekretarieti ya Kituo cha Usuluhishi kianze kuandaliwa mapema ili jengo litakapokuwa limekamilika lianze kufanya kazi mara moja.