Tumieni Samia Legal Aid Kutoa Haki - RC Mtanda

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewasihi viongozi wa Mkoa huo kuendelea kutoa haki kwa wananchi bila upendeleo ili kuwaletea wananchi hao Maendeleo.
Mhe. Mtanda amesema hayo Februari 18, 2025 Jijini Mwanza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign).
Kampeni hiyo itakuwepo Jijini Mwanza kwa siku 9 baada ya Uzinduzi ambapo Jopo la wataalamu wa sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria litakua likitoa huduma hiyo katika Halmashauri zote za Jiji la Mwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Alfred Dede akitoa salamu za Wizara kwa Niaba ya Katibu Mkuu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Februari 18, 2025 Jijini Mwanza.