Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

WAZIRI CHANA AFANYA KIKAO CHA KIMKAKATI NA MENEJIMENTI YA WIZARA

Imewekwa: 24 Jan, 2024
WAZIRI CHANA AFANYA KIKAO CHA KIMKAKATI NA MENEJIMENTI YA WIZARA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.  Balozi Dkt. Pindi Chana amefanya kikao na Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na kupokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 24 Januari, 2024 katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma kikiwa na malengo ya kutathmini kwa kina utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa nusu muhura wa bajeti ya mwaka 2023/ 2024.

Mhe. Waziri Chana ameiopongeza Menejimenti na watumishi wote kwa ujumla kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuhakikisha kazi za kuwahudumia wanachi zinakwenda vizuri na kwa wakati.

Akiongea kwenye kikao hicho Waziri Chana amesema “natambua jukumu la kutekeleza majukumu haya ni kubwa lakini lazima tuongeze kasi ya kujituma zaidi kuhakisha tunatimiza adhima ya Mhe Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia watanzania ikiwemo kutatua kero mbalimbali”.