TAARIFA KWA UMMA KUTEULIWA KATIKA ORODHA YA WAJUMBE WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA UTATUZI WA MIGOGORO YA UWEKEZAJI (ICSID) KUTOKA TANZANIA KATIKA ORODHA YA WASULUHISHI NA WAENDESHA MARIDHIANO
Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji (International Centre for Settlement of Investment Disputes – ICSID) kimeteua wataalamu saba kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wajumbe kwenye Orodha za Wasuluhishi na Waendesha Maridhiano wa Kituo hicho. Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) ni taasisi ya kimataifa inayojihusisha na utatuzi wa migogoro ya uwekezaji.
Uteuzi huo ambao utaendelea hadi tarehe 2 Juni 2032, unaakisi dhamira endelevu ya Tanzania ya kuimarisha ushiriki wake katika mifumo ya kimataifa ya utatuzi wa
migogoro ya uwekezaji na kukuza utawala wa sheria katika masuala yanayohusu uwekezaji na maendeleo ya uchumi.
Wajumbe walioteuliwa ni:
Orodha ya Wasuluhishi (Arbitrators)
1. Bw. George Nathaniel Mandepo;
2. Prof. Clement Julius Mashamba; na
3. Jaji Mstaafu Dkt. Fauz Abdallah Twaib.
Orodha ya Waendesha Maridhiano (Concilliators)
1. Ndg. Nuhu Sadiki Mkumbukwa;
2. Prof. Saudin Jacob Mwakaje;
3. Jaji Mstaafu Dkt. Atuganile Florida Ngwala; na
4. Ndg. Sabho Nyakore Wambura.
Uteuzi huu unatambua umahiri wao wa kitaaluma, uadilifu na mchango wao katika maendeleo ya sheria na utatuzi wa migogoro nchini na kimataifa.
Wizara inawapongeza wajumbe wote walioteuliwa na kuwatakia mafanikio wanapotekeleza jukumu hili muhimu la kuendeleza utatuzi wa migogoro ya uwekezaji
kwa misingi ya haki, usawa, ufanisi na kutopendelea upande wowote.
Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
24 Juni, 2026.
Katiba na Sheria www.sheria.go.tz