JAJI MKUU NA KATIBU MKUU WAJADILIANA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA HAKI
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Masaju amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Shekalaghe, wakati alipomtembelea katika Makao Makuu ya Mahakama,Tambukareli jijini Dodoma Julai 15, 2026.
Katika kikao hicho viongozi hao walijadiliana kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Katiba na Sheria na Mahakama katika kutekeleza majukumu yao ya kikatiba.
Majadiliano hayo pia yamelenga katika kuweka mikakati ya pamoja ya kuendeleza upatikanaji wa Haki ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa huduma za kimahakama kwa ubora na kwa wakati kwa Wananchi.
Viongozi waliohudhuria katika kikao hicho ni pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Dkt. John Jingu, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Siyani, pamoja na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya.