TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA
27 Nov, 2025
Wizara ya Katiba na Sheria inapenda kuwatangazia watu wenye nia ya kutoa Huduma za Usuluhishi, Maridhiano, Majadiliano na Upatanishi ambao wanakidhi vigezo kwa mujibu wa Kanuni; kuwasilisha maombi yao pamoja na kuambatisha nyaraka kwenye Portal ya HAKI SHERIA (https://tlegalaid.sheria.go.tz). Kwa mwombaji mpya ingia eneo la MTATUZI WA MIGOGORO kisha bonyeza Sajili. Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na Ofisi ya Msajili kupitia msajili.mmuu@sheria.go.tz au simu namba 0714237904. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 09 Januari, 2026.