TANGAZO LA NAFASI ZA UTEUZI
Ibara ya 129 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 katika Sura ya Sita, Sehemu ya Kwanza inaanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Kwa kuwa muda wa kuhudumu wa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora umefika mwisho, Kamati ya Uteuzi iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 129 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba kujaza nafasi wazi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Makamishna na Makamishna Wasaidizi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kama ifuatavyo:-
1.0 NAFASI: MWENYEKITI (NAFASI 1)
1.1 Sifa za Mwombaji:-
Kwa mujibu wa Ibara ya 129 (2) (a), ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 mwombaji atakuwa ni mtu mwenye sifa ya kuweza kuteuliwa kuwa Jaji;
1.2 Uzoefu Unaohitajika
Kwa kuzingatia kanuni ya 4 (4) (a – i), ya Kanuni za THBUB (Utaratibu wa Uteuzi wa Makamishna), 2018 mwombaji anatakiwa kuwa na:-
- Maarifa, uzoefu na ushiriki katika masuala yanayohusiana na sheria, utawala, siasa na mambo ya kijamii;
- Sifa za hali ya juu zinazohusiana na maadili, uadilifu, kutokuwa na upendeleo na kuwa mahiri kwenye masuala ya haki za binadamu na utawala bora;
- Kujitoa kwa hali ya juu kwenye masuala ya haki za binadamu na maadili;
- Uwezo na ujuzi mkubwa wa kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza fasaha;
- Uwezo wa kuwa na mizania inayolingana katika masuala ya haki na kutenda bila upendeleo na kutoa maamuzi sahihi kwa haraka na awe na uwezo wa kuyaandika na kuyasema;
- Uwezo wa kushughulikia hali ngumu na zenye changamoto za kihisia kwa busara na ustadi wa kidiplomasia;
- Uwezo wa kushughulikia masuala nyeti ya kijamii, kisiasa na malalamiko kwa usiri inapohitajika;
- Ujuzi wa hali ya juu wa kutatua migogoro; na
- Uwezo wa kufanya kazi ipasavyo kwa ushirikiano na binafsi.
1.3 Majukumu
- Kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi;
- Kufanya shughuli za kupokea malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu kwa jumla;
- Kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
- Kufanya utafiti, kutoa na kueneza nchini elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
- Kama ikibidi, kufungua mashauri mahakamani ili kuzuia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu au kurekebisha haki inayotokana na uvunjwaji huo wa haki za binadamu, au ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
- Kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika au taasisi yoyote inayohusika katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake au utekelezaji unaokiuka madaraka hayo;
- Kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na vya sekta ya binafsi kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
- Kuchukua hatua zipasazo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza usuluhishi na suluhu miongoni mwa watu na taasisi mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbele ya Tume.
1.4 Ngazi ya Mshahara:
Kiwango cha LSSE/8 -1 na kupatiwa nyongeza ya kuvutia na motisha.
2. NAFASI: MAKAMU MWENYEKITI (NAFASI 1)
2.1 Sifa za Mwombaji
Kwa mujibu wa Ibara ya 129 (2) (c), ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 mwombaji anatakiwa awe mtu mwenye ujuzi, uzoefu na upeo mkubwa katika mambo ya haki za binadamu, sheria, utawala, siasa au mambo ya jamii.
2.2 Uzoefu Unaohitajika
Kwa kuzingatia kanuni ya 4 (4) (a – i), ya Kanuni za THBUB (Utaratibu wa Uteuzi wa Makamishna), 2018 mwombaji anatakiwa kuwa na:-
- Maarifa, uzoefu na ushiriki katika masuala yanayohusiana na sheria, utawala na mambo ya kijamii;
- Sifa za hali ya juu zinazohusiana na maadili, uadilifu, kutokuwa na upendeleo na kuwa mahiri kwenye masuala ya haki za binadamu na utawala bora;
- Kujitoa kwa hali ya juu kwenye masuala ya haki za binadamu na maadili;
- Uwezo na ujuzi mkubwa wa kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza fasaha;
- Uwezo wa kuwa na mizania inayolingana katika masuala ya haki na kutenda bila upendeleo na kutoa maamuzi sahihi kwa haraka na awe na uwezo wa kuyaandika na kuyasema;
- Uwezo wa kushughulikia hali ngumu na zenye changamoto za kihisia kwa busara na ustadi wa kidiplomasia;
- Uwezo wa kushughulikia masuala nyeti ya kijamii, kisiasa na malalamiko kwa usiri inapohitajika;
- Ujuzi wa hali ya juu wa kutatua migogoro; na
- Uwezo wa kufanya kazi ipasavyo kwa ushirikiano na binafsi.
2.3 Majukumu:
- Kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi;
- Kufanya shughuli za kupokea malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu kwa jumla;
- Kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
- Kufanya utafiti, kutoa na kueneza nchini elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
- Kama ikibidi, kufungua mashauri mahakamani ili kuzuia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu au kurekebisha haki inayotokana na uvunjwaji huo wa haki za binadamu,au ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
- Kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika au taasisi yoyote inayohusika katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake au utekelezaji unaokiuka madaraka hayo;
- Kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na vya sekta ya binafsi kuhusu haki za binadamu na utawala bora; na
- Kuchukua hatua zipasazo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza usuluhishi na suluhu miongoni mwa watu na taasisi mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbele ya Tume.
2.4 Ngazi ya Mshahara
Kiwango cha LSSE/7 -1 na kupatiwa nyongeza ya kuvutia na motisha.
3 NAFASI: MAKAMISHNA (NAFASI 5)
3.1 Sifa za Mwombaji:-
Kwa mujibu wa Ibara ya 129 (2) (c), ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 mwombaji anatakiwa awe mtu mwenye ujuzi, uzoefu na upeo mkubwa katika mambo ya haki za binadamu, sheria, utawala, siasa au mambo ya jamii
3.2 Uzoefu Unaohitajika
Kwa kuzingatia kanuni ya 4 (4) (a – i), ya Kanuni za THBUB (Utaratibu wa Uteuzi wa Makamishna), 2018 mwombaji anatakiwa kuwa na:-
- Maarifa, uzoefu na ushiriki katika masuala yanayohusiana na sheria, utawala na mambo ya kijamii;
- Sifa za hali ya juu zinazohusiana na maadili, uadilifu, kutokuwa na upendeleo na kuwa mahiri kwenye masuala ya haki za binadamu na utawala bora;
- Kujitoa kwa hali ya juu kwenye masuala ya haki za binadamu na maadili;
- Uwezo na ujuzi mkubwa wa kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza fasaha;
- Uwezo wa kuwa na mizania inayolingana katika masuala ya haki na kutenda bila upendeleo na kutoa maamuzi sahihi kwa haraka na awe na uwezo wa kuyaandika na kuyasema;
- Uwezo wa kushughulikia hali ngumu na zenye changamoto za kihisia kwa busara na ustadi wa kidiplomasia;
- Uwezo wa kushughulikia masuala nyeti ya kijamii, kisiasa na malalamiko kwa usiri inapohitajika;
- Ujuzi wa hali ya juu wa kutatua migogoro; na
- Uwezo wa kufanya kazi ipasavyo kwa ushirikiano na binafsi.
3.3 Majukumu:-
- Kuhamasisha nchini hifadhi ya haki za binadamu na wajibu kwa jamii kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi;
- Kufanya shughuli za kupokea malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu kwa jumla;
- Kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
- Kufanya utafiti, kutoa na kueneza nchini elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
- Kama ikibidi, kufungua mashauri mahakamani ili kuzuia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu au kurekebisha haki inayotokana na uvunjwaji huo wa haki za binadamu,au ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;
- Kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika au taasisi yoyote katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake au utekelezaji unaokiuka madaraka hayo;
- Kutoa ushauri kwa Serikali na vyombo vingine vya umma na vya sekta ya binafsi kuhusu haki za binadamu na utawala bora;
- Kuchukua hatua zipasazo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza usuluhishi na suluhu miongoni mwa watu na taasisi mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbele ya Tume.
3.4 Ngazi ya Mshahara:-
- Kiwango cha LSSE/6 -1 na kupatiwa nyongeza ya kuvutia na motisha.
4 NAFASI: MAKAMISHNA WASAIDIZI
4.1 Sifa za Mwombaji
Kwa mujibu wa kifungu cha 7 (3) cha Sheria ya THBUB Sura ya 391 mwombaji anatakiwa awe mtu mwenye sifa njema na anafahamika kwa kuwa mwenye maadili ya juu, uadilifu, kutopendela na mahiri katika masuala ya haki za binadamu na utawala bora.
4.1 Uzoefu Unaohitajika
Kwa kuzingatia kanuni ya 4 (4) (a – i), ya Kanuni za THBUB (Utaratibu wa Uteuzi wa Makamishna), 2018 mwombaji anatakiwa kuwa na:-
- Maarifa, uzoefu na ushiriki katika masuala yanayohusiana na sheria, utawala na mambo ya kijamii;
- Sifa za hali ya juu zinazohusiana na maadili, uadilifu, kutokuwa na upendeleo na kuwa mahiri kwenye masuala ya haki za binadamu na utawala bora;
- Kujitoa kwa hali ya juu kwenye masuala ya haki za binadamu na maadili;
- Uwezo na ujuzi mkubwa wa kuandika na kuongea Kiswahili na Kiingereza fasaha;
- Uwezo wa kuwa na mizania inayolingana katika masuala ya haki na kutenda bila upendeleo na kutoa maamuzi sahihi kwa haraka na awe na uwezo wa kuyaandika na kuyasema;
- Uwezo wa kushughulikia hali ngumu na zenye changamoto za kihisia kwa busara na ustadi wa kidiplomasia;
- Uwezo wa kushughulikia masuala nyeti ya kijamii, kisiasa na malalamiko kwa usiri inapohitajika;
- Ujuzi wa hali ya juu wa kutatua migogoro; na
- Uwezo wa kufanya kazi ipasavyo kwa ushirikiano na binafsi.
4.2 Majukumu
- Kupokea malalamiko kutoka kwa umma;
- Kufanya uchunguzi wa papo hapo kama inavyoweza kuhitajika; na
- Kutekeleza kazi nyingine zinazohusiana na majukumu ya THBUB kama atakavyopangiwa na THBUB.
4.3 Ngazi ya Mshahara
Kiwango cha LSSE4 na kupatiwa nyongeza ya kuvutia na motisha.
5.0 MASUALA MENGINE YA KUZINGATIA
5.1 MUDA NA MASHARTI YA KAZI
- Kwa kuzingatia Ibara ya 129 (5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wengine wote, kila mmoja atashika madaraka yake kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja tu cha miaka mitatu (3);
- Vilevile, Ibara ya 129 (6) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya THBUB, Sura ya 391, inaelekeza kuwa, kwa madhumuni ya kuwakinga Makamishna kutokana na migongano ya kimaslahi, mtu yeyote akiteuliwa kuwa Kamishna wa THBUB atalazimika kuacha mara moja madaraka yoyote katika chama chochote cha siasa, au madaraka ya aina nyingine yoyote kama vile: Ubunge; Ujumbe katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar; Spika wa Bunge; Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar; Jaji au wadhifa mwingine wa kimahakama; Utumishi Serikalini; Ujumbe wa Tume ya Uchaguzi; Ujumbe katika mamlaka ya Serikali za Mitaa na utumishi wowote katika mamlaka ya serikali za mtaa; au nafasi yoyote nyingine katika utumishi wa umma.
5.2 NAMNA YA KUOMBA
Barua zote za maombi zinapaswa kuambatana na wasifu wa kina, nakala za vyeti vya taaluma/elimu na barua tatu za mapendekezo kutoka kwa wadhamini ambazo zitatumwa kwa Kamati ya Uteuzi, Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Eneo la Mtumba, S. L. P. 1954, Dodoma, au barua pepe: kamati.uteuzi@oag.go.tz. Kwa watakaowasilisha kwa mkono, kwa upande wa Tanzania Bara barua zitapokelewa Jengo la Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizopo Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Eneo la Mtumba Dodoma. Aidha, kwa upande wa Zanzibar barua zitawasilishwa kwa mkono katika Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizopo Shehia ya Mombasa Barabara ya Mkapa Mtaa wa Tawin Jengo Na.MS/ML/F199 Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi itakuwa siku 21 tangu tarehe ya kwanza ya kutangazwa kwa Tangazo hili, yaani, kabla au ifikapo tarehe 31 Agosti, 2026.
5.3 TAARIFA NA UCHAPISHAJI WA MAJINA YA WAOMBAJI WALIOKIDHI VIGEZO
Kwa mujibu wa Kanuni ya 7(1) ya Kanuni za THBUB (Utaratibu wa Uteuzi wa Makamishna), 2018 majina ya waombaji wote waliokidhi vigezo na kuitwa kwenye usaili yatatangazwa kwenye vyombo vya habari ambapo umma utaalikwa kuwasilisha maoni kwa Kamati ya Uteuzi, Mtaa wa Utumishi, Mji wa Serikali Eneo la Mtumba, S. L. P. 1954, Dodoma, au barua pepe: kamati.uteuzi@oag.go.tz ndani ya siku ishirini na moja, (21) iwapo waombaji wanastahili kushika nafasi hizo. Kamati ya Uteuzi inaweza kuzingatia maoni yaliyowasilishwa kutoka kwa umma.
Waombaji waliokidhi vigezo watajulishwa tarehe na mahala watakapofanyiwa usaili na Kamati ya Uteuzi.
Kwa ufafanuzi wowote piga simu namba 0733122200.
Imetolewa na:
NAIBU MWANASHERIA MKUU
KATIBU
KAMATI YA UTEUZI