TAARIFA KWA UMMA: UWEPO WA MATAPELI WANAOPIGA SIMU NA KUJITAMBUSHA KUWA NI WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA
Wizara ya Katiba na Sheria imepokea taarifa ya kuwepo kwa mtu anayepiga simu kwa Namba 0623 728 828 na kujitambulisha kwa jina la Dkt. Juma Zuberi Homera Waziri na Katiba na Sheria akiomba atumiwe fedha kwa njia ya udanganyifu.
Wizara inatoa taarifa kuwa Waziri Dkt. Juma Zuberi Homera hajawahi kumpigia mtu yeyote simu kwa namba hiyo lengo la kumuomba fedha hivyo wananchi wanapaswa kufahamu kwamba namba hiyo sio ya Waziri wa Katiba na Sheria na mtu huyo ni tapeli mwenye lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Aidha, tunapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa makini na utapeli huo na kuripoti namba hiyo mara tu wanapopigiwa kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno UTAPELI kwenda Namba 15040. Taarifa yako itashughulikiwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Mtoa Huduma husika.
Wananchi pia wanaweza kutoa taarifa za utapeli huo kwa Wizara ya Katiba na Sheria kwa kupiga Namba 0800-004-004 au 0262-160-360 au kwa WhatsApp Namba 0739 101 910.
IMETOLEWA Na,
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA.