Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Mradi wa e-Justice

Mradi huu unalenga kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika Sekta ya Sheria na kuunganisha mifumo ya taasisi ya utoaji huduma za kisheria kwa njia za kielektroni ili kuongeza ufanisi, kuharakisha upatikanaji wa haki na kupunguza gharama za utoaji wa huduma hizo. Matokeo ya awali ya mradi huu ni kuwa na mifumo iliyoainishwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa Taasisi za Haki Jinai nchini. Matokeo ya Kati ya Mradi huu ni kuwezesha haki Jinai kupatikana kwa wakati nchini. Matokeo ya muda mrefu ni kuwa na Mfumo wa haki jinai unaochangia maendeleo endelevu ya nchi.