Bi. Akisa Mhando, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, Wizara ya Katiba na Sheria, akifungua rasmi kikao kazi cha kuwajengea uelewa waandishi wa habari na Wahariri juu ya Sheria ya Watoa Taarifa na Mashahidi Sura namba 446 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Zabibu Hotel, Oktoba 27, 2025.
Picha ya pamoja ya wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Waandishi wa Habari na Wahariri kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria kikao kazi cha kujengeana uelewa kuhusu Sheria ya Watoa Taarifa na Mashahidi Sura namba 446
Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Judica Emmanuel Nkya akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Watoa Taarifa na Mashahidi, sura namba 446 katika kikao kazi cha kuwajengea uelewa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari, kikao kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano Zabibu Hoteli jijini Dodoma, Oktoba 27, 2025.