Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
Malengo:
Kutoa huduma za kitaalamu katika manunuzi, uhifadhi na huduma za ugavi.
kitengo hiki kitatekeleza shughuli zifuatazo:
- Kuandaa Mpango wa Manunuzi wa Mwaka wa Wizara.
- Kushauri menejimenti kuhusu masuala yanayohusu manunuzi ya bidhaa na huduma na usimamizi wa vifaa.
- Kufuatilia uzingatiaji wa mchakato na taratibu za manunuzi kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma.
- Kununua, kutunza na kusimamia vifaa na huduma za ugavi ili kusaidia mahitaji ya ugavi wa wizara.
- Kufuatilia usambazaji wa vifaa vya ofisi.
- Kudumisha na kuhuisha orodha ya bidhaa na vifaa.
- kutoa huduma za sekretarieti kwa bodi ya zabuni ya wizara kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma.
- kuweka vipimo/viwango vya bidhaa na huduma zinazonunuliwa na kufuatilia thamani ya fedha.