Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Tume ya Utumishi wa Mahakama

1.0 Utangulizi

Tume ya Utumishi wa Mahakama imeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yam waka 1977 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uendashaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011.

Wajumbe wa Tume ni pamoja na:

  1.  Jaji Mkuu ambaye ni Mwenyekiti
  2. Mwanasheria Mkuu wa Serikali
  3. Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani
  4. Jaji Kiongozi
  5. Wajumbe wawili ambao wanateuliwa na Rais

Kwa mujibu wa Kifungu Na. 15 cha Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 15 (1) cha sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011. Mtendaji Mkuu wa Mahakama ndiye Katibu wa Tumen a mtekelezaji wa maamuzi ya Tume.

2.0 Historia ya Tume

Kaba ya kutungwa kwa Sheria ya Utumishi wa Mahakama Na. 2 ya mwaka 2005, na sasa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011, kulikuwa na Tume mbili zilizokuwa zinashughulikia watumishi wa Mahakama yaani Tume ya Utumishi wa Mahakama iliyokuwa inashughulikia Mahakimu Wakazi na Mahakimu wa wilaya na Tume maalum ya Utumishi wa Mahakama iliyokuwa inashughulikia Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo.

Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama walioainishwa ndani ya Katiba na wajumbe wa Tume maalum walioainishwa kwenye Sheria ya Utumishi wa Mahakama.

Kwa sasa masuala yote ya kiutumishi kwa Watumishi wa Mahakama yanashughulikiwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama, ambayo wajumbe na majukumu yake vimeainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011. Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama inaelekeza kuhusu kuwepo kwa Kamati za Maadili ya Mahakimu katika ngazi ya Mikoa ana Wilaya ambazo kazi yake ni kuchunguza malalamiko dhidi ya Mahakimu.

 3.0 Dira ya Tume

“Kuwa kitovu cha ubora katika kusimamia Utumishi wa Mahakama Tanzania bara.

4.0 Dhima

“Utoaji endelevu wa huduma ya ushauri na usimamizi wa Rasilimali watu katika Utumishi wa Mahakama Tanzania Bara”

Maadili Msingi

  i.  Uadilifu;

  ii. Uwazi

  iii. Uwajibikaji

  iv. Ushirikiano

  v. Weledi

  vi. Usiri

5.0 Majukumu ya Tume ya Utumishi wa Mahakama

Mamlaka ya Tume ya Utumishi wa Mahakama kama chombo cha kusimamia ajira na nidhamu za watumishi wa Mahakama yanatokana na Ibara ya 113 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Toleo la mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu Na. 29 (1) cha Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011 kama ifuatavyo;

a)  Kumshauri Mhe. Rais kuhusu;

i.  Uteuzi wa Jaji Kiongozi pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

ii. Uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu, Msajili wa Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu,

iii. Kutokuwa na uwezo kwa Jaji wa Rufaa, Jaji wa Kiongozi wa Mahakama Kuu kutekeleza majukumu ya ofisi,

iv. Mwenendo usioridhisha wa Jaji wa Rufaa, Jaji Kiongozi, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu, Msajiliwa Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu,

  v. Maslahi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania.

b) Kuchambua lalamiko dhidi ya Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi au Afisa yeyote wa Mahakama,

 c)  Kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi, au Jaji mbali na hatua zilizoainishwa katika Katiba,

 d)  Kuteua, Kupandisha Cheo na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wote isipokuwa kwa wale ambao sio mamlaka ya uteuzi wa Tume,

 e) Kuajiri na Kupandisha cheo au kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mtumishi yeyote ambaye si Afisa wa Mahakama kama ilivyoainishwa katika sheria.

5.1 Uwepo wa Kamati za Maadili ya Maafisa wa Mahakama

Kifungu cha 36 cha Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na.4 ya mwaka 2011 kinaelekeza kuwepo kwa kamati za Maadili katika ngazi mbalimbali ambazo zitahusika na uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili dhidi ya Maafisa wa Mahakama ambazo ni;

        i.  Kamati ya Maadili ya Majaji (Judges Ethics Committee)

        ii.  Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Mahakama (Judicial Offgicers Ethics Committee)

       iii.  Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Mahakama ya mkoa

       iv.  Kamati ya Maadili ya Maafisa wa Mahakama ya wilaya

    v.  Kifungu cha 14 (2) cha Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011, kimeruhusu kuwepo kwa kamati ya ushauri ya Ajira. Kamati hii itasaidia kuishauri Tume kuhusu masuala ya Ajira, Kuthibitishwa kazini, kupandishwa vyeo pamoja na nidhamu kwa watumishi wasio Maafisa wa Mahakama.

6.0 Uimarishaji wa Kamati za Maadili

Pamoja na majukumu ya Tume kama yalivyoainishwa hapo juu, ili kuimarisha maadili ya Maafisa wa Mahakama, Tume inao wajibui wa kuziimarisha Kamati za Maadili kwa kuzijengea uwezo ili ziweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.