Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

1 UTANGULIZI

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeanzishwa kama Ofisi huru ya Umma kupitia Tangazo la Serikali Na.49 la mwaka 2018 la tarehe 13 Februari, 2018 la kuanzisha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kutekeleza mamlaka ya Kikatiba aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye anatoa mchango mkubwa katika kusimamia haki jinai.   Kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Mkurugenzi wa Mashtaka amepewa uwezo na mamlaka ya kusimamia uendeshaji wa mashtaka yote ya jinai katika Mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi.   Kwa msingi huo, Mkurugenzi wa Mashtaka ana uwezo wa kufungua, kuendesha na kusimamia mashtaka yote ya jinai nchini.   Kutokana na Ibara hiyo ya Katiba, Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka hayamhusu mtu mwingine yoyote au mamlaka nyingine na hawajibiki kusimamiwa na mtu mwingine yoyote au mamlaka nyingine.   Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurugenzi wa Mashtaka anatakiwa kufuata kanuni zifuatazo:  Kutenda haki; Kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria; na maslahi ya umma.   Nafasi hii imewekwa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Taifa ya Mashtaka, Sura ya 430.

Tangazo la Serikali Na.49 la mwaka 2018 limeweka mpangilio wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, muundo wake, utawala, ufuatiliaji usimamizi wa mashtaka na namna uratibu wa upelelezi utakavyokuwa kwa lengo la kukuza na kuinua utendaji haki jinai na masuala yanayohusiana nayo.

DIRA NA DHIMA

DIRA

Haki, amani na usalama kwa maendeleo ya Taifa.

DHIMA

Kushirikiana na wadau na kuendesha kesi bila woga, upendeleo ili kuhakikisha uwepo wa   haki, amani, na usalama katika jamii.

MAADILI YA MSINGI

Maadili ya Msingi ni-

  1. Uwajibikaji:  Kuwajibika katika utekelezaji wa majukumu kwa wakati;
  2. Kukubalika:  Uthabiti na uwezo wa kuaminika na kuthaminiwa;
  3. Uadilifu: Kwa maadili na uaminifu bila kuvumilia vitendo vya rushwa na                         ubadhirifu;
  4. Uweledi:  Kwa kujituma, kujitoa, umahili na utaalamu ndani na nje ya ofisi;
  5. Huduma bora: Kwa kutoa huduma bora kwa kufanya kazi pamoja, heshima na adabu.

2.  MAJUKUMU NA WAJIBU

MKURUGENZI WA MASHTAKA

Mkurugenzi wa Mashtaka ni mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Mkurugenzi wa Mashtaka ndiye msimamizi mkuu wa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Mawakili wa serikali na Waendesha Mashtaka katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa ni:

  1. Kuamua kushtaki au kutoshtaki kwenye makosa ya jinai;
  2. Kuanzisha, kuendesha na kusimamia mashtaka ya makosa ya jinai katika mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi;
  3. Kutwaa na kuendelea na mashtaka ya kesi yoyote ya jinai iliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine;
  4. Kufuta mahakamani mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine katika hatua yoyote kabla hukumu kutolewa;
  5. Kutoa maagizo kwa jeshi la polisi au vyombo chunguzi vyoyote kuchunguza taarifa yoyote ya kijinai na kutoa taarifa kwake haraka inavyowezekana;
  6. Kuchukua hatua muhimu kwa jambo lolote lenye tija katika mashtaka ya jinai;
  7. Kutoa miongozo inayohusu uratibu wa upelelezi na uendeshaji mashtaka;
  8. Kuteua na kutengua mamlaka ya waendesha mashtaka wa umma;
  9. Kumshauri waziri mwenye dhamana katika masuala ya mashtaka yanayohitaji sera au hatua za kibunge;
  10. Kuteuwa maafisa maalum ndani ya taasisi za serikali kusimamia mali zilizozuiliwa au kutaifishwa na mahakama katika mazingira ambayo ni vigumu kuteua wasii;
  11. Kufanya kazi nyingine ambayo zinahusiana na mashtaka ya umma;
  12. Kuwasimamia maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine walioteuliwa au kuajiriwa na ofisi ya taifa ya mashtaka;
  13. Kusimamia shughuli zote zinazofanywa na maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka;
  14. Kuita afisa yoyote wa umma kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na jambo lolote ambalo linahusu mashtaka ya umma;
  15. Kuandaa na kuwasilisha kwa waziri taarifa ya nusu mwaka na nakala kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya taifa ya mashtaka; na
  16. Kuteua au kuajiri na kuwajibisha maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka.

NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Mkurugenzi wa Mashtaka na atafanya majukumu yake kadri atakavyoelekezwa na Mkurugenzi wa Mashtaka. Aidha Naibu Mkurugenzi wa mashtaka atakuwa ndiye afisa masuuli wa taasisi na atasimamia shughuli za kila siku za taasisi na atakuwa mamlaka ya nidhamu ya watumishi kwa mujibu wa kanuni na sheria za utumishi wa umma. Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ataandaa kanuni za nidhamu kwa waendesha mashtaka na kuhakikisha viwango vya kimataifa vinazingatiwa na ndiye atatunza kumbukumbu za waendesha mashtaka wa umma.

DIVISHENI YA UTENGANISHAJI WA SHUGHULI ZA MASHTAKA NA UPELELEZI                        

Lengo: kutoa ushauri wa kitaalamu na huduma za uendeshaji mashtaka nchini.

Majukumu:

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

  1. Kuratibu utekelezaji wa programu ya uendeshaji wa mashtaka;
  2. Kuratibu na kuandaa miongozo inayohusu upelelezi na uendeshaji kesi za jinai;
  3. Kusimamia ukaguzi, ufatiliaji na ubora wa huduma zinazotolewa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka;
  4. Kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa miongozo inayotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka kuhusiana na upelelezi na uendeshaji mashtaka ya jinai;
  5. Kuratibu upelelezi ili kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwaa na mwendesha mashtaka
  6. Kuratibu na kusimamia matumizi bora ya mwongozo wa waendesha Mashtaka na Mwongozo wa Wapelelezi;
  7. Kuandaa mahitaji ya mafunzo ya kisheria ili kuleta tija katika mashtaka;
  8. Kuratibu ukaguzi wa sero za polisi na magereza;
  9. Kuratibu ufuatiliaji wa majukumu waliyopangiwa kwa watumishi na maafisa wengine ndani ya taasisi;
  10. Kutafuta ufumbuzi wa masuala ya kisheria yanayotokana na maamuzi ya mahakama ambayo yanahitaji utekelezaji wa wadau wengine;
  11.      Kushirikisha wadau   wa haki jinai katika   masuala ya kesi za jinai;
  12. Kuratibu ukusanyaji wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kuhusiana na kesi zinazoendelea au kuisha   ili kuleta tija katika uendeshaji wa kesi za jinai;
  13. Kuratibu uchambuzi wa taarifa zilizokusanywa;
  14. Kuratibu ukusanyaji taarifa za mashauri ya jinai, kuchambua kitakwimu ili kupata taarifa zitakazosaidia kuleta tija katika mashtaka na hivyo kupunguza makosa ya jinai;
  15. Kufungua   kuendesha na kusimamia   mashtaka na
  16. Kusimamia rufaa na maombi ya jinai mahakamani kwa niaba ya Jamhuri.

Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu tatu (3) zifuatazo:

  1. Sehemu ya uendeshaji mashtaka;
  2. Sehemu ya usimamizi wa   mashtaka mahakamani; na
  3. Sehemu ya makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa Taifa.

DIVISHENI YA UTAIFISHAJI MALI, MAKOSA YANAYOVUKA MIPAKA NA UHALIFU MAHSUSI

Lengo: kutoa utaalamu na huduma ya kunyang’anya wahalifu au washirika wao faida zitokanazo na vitendo vya uhalifu pamoja na kuendesha kesi hizo mahakamani.   

Majukumu:

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

  1. Kuratibu utekelezaji wa sheria pamoja na masuala yote yahusuyo utaifishaji na urejeshaji   mali zitokanazo na uhalifu;
  2. Kufuatilia na kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi zinazohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika kutenda uhalifu na mazalia yake;  
  3. Kuratibu tathmini ya ufanisi wa sheria, kanuni, miongozo na viwango kwenye masuala ya utaifishaji na urejeshaji mali zitokanazo na uhalifu na kupendekeza marekebisho yake;
  4. Kuratibu utambuzi na ufuatiliaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu   na mazalia yake;
  5. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kimataifa na kikanda katika ufuatiliaji, utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake;
  6. Kufuatilia na kusimamia utambuzi wa kesi zenye uwezekano wa kuwa na mali za kurejesha;
  7. Kufuatilia na kusimamia mali zilizozuiliwa, taifishwa na kurejeshwa;
  8. Kutoa ushauri na muongozo kuhusu maombi ya utaifishaji na urejeshaji wa mali zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake, yanayoombwa kwa au na    jamhuri ya muungano wa tanzania;
  9. Kuratibu, kutathimini na kushauri ufanisi wa sera, sheria, kanuni, miongozo na viwango vya usimamizi wa makosa yanayovuka mipaka na kupangwa;
  10. Kuratibu na kutoa miongozo kwa mamlaka zinazotekeleza sheria katika masuala yahusuyo makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
  11. Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za makosa yanayovuka mipaka na kupangwa katika ngazi za   mikoa na wilaya;
  12. Kufungua na kuendesha kesi za makosa yanayovuka mipaka, ya kupangwa na masuala yanayohusiana nayo;
  13. Kusimamia mapitio ya majalada yanayohusiana na makosa yanayovuka mipaka   na ya kupangwa toka vyombo chunguzi;
  14. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda   pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
  15. Kuratibu na kusimamia masuala yanayohusu ubadilishanaji wa wahalifu watoro kama itakavyoelekezwa na waziri mwenye dhamana na masuala ya sheria;
  16. Kushauri kwenye masuala ya ushirikiano wa kesi za jinai;
  17. Kusimamia uendeshaji wa kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
  18. Kuwezesha uhudhuriaji wa mashahidi kutoka na kwenda nje ya nchi kutoa ushahidi;
  19. Kuratibu na kutoa miongozo kwa mamlaka zinazotekeleza sheria katika masuala ya makosa ya kimtandao;
  20. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda   pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa ya kimtandao; na
  21. Kuratibu na kushauri ufanisi katika uendeshaji wa kesi za makosa ya kimtandao.

Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na Sehemu tatu (3) kama ifuatavyo:

  1. Sehemu ya utaifishaji na urejeshaji   mali;
  2. Sehemu ya Makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa; na
  3. Sehemu ya Makosa ya kimtandao.

DIVISHENI YA MAKOSA YA UDANGANYIFU, UTAKATISHAJI FEDHA NA RUSHWA

Lengo: kutoa utaalamu na huduma ya mashtaka kwa makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha, rushwa, mazingira na mali asili.

Majukumu

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

  1. Kupitia na kutoa ushauri kwenye sera. Sheria, kanuni, miongozo na viwango katika usimamizi wa makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha   na rushwa;
  2. Kuratibu kesi za rushwa katika mahakama kuu kitengo cha makosa ya rushwa na uhujumu uchumi   na mahakama za chini;
  3. Kuratibu taasisi zinazotekeleza sheria katika   makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha, rushwa na masuala yanayohusiana nayo;
  4. Kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za udanganyifu na rushwa katika ngazi za mikoa na wilaya;
  5. Kufungua na kuendesha kesi za rushwa na udanganyifu;
  6. Kusimamia mapitio ya majalada ya kesi za utakatishaji fedha, rushwa na udanganyifu;
  7. Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na   wadau katika kupambana na   makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa;
  8. Kusimamia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa; na
  9. Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na rushwa na udanganyifu.

Divisheni   hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu (3) kama ifuatavyo:

  1. Sehemu ya makosa ya   udanganyifu na utakatishaji fedha;
  2. Sehemu ya makosa ya rushwa; na
  3. Sehemu ya mazingira na mali asili.

DIVISHENI YA USIMAMIZI WA KESI NA URATIBU WA UPELEZI

Lengo: kutoa utaalamu katika usimamizi wa kesi na uratibu wa upelelezi.

Majukumu:

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

  1. Kutoa maelekezo katika usimamizi, ukaguzi na ufuatiliaji wa ubora katika uendeshaji wa huduma zinazotolewa na Ofisi;
  2. Kusimamia mahitaji ya mafunzo katika masuala ya sheria kwa vitendo pamoja na usimamizi wa taarifa   ili kuhakikisha ufanisi katika uendeshaji kesi;
  3. Kusimamia utendaji kazi wa kila mwendesha mashtaka, majukumu ya Jukwaa la Taifa la Haki Jinai, Kamati za kusimamia kesi na kuandaa ripoti na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka;
  4. Kutekeleza mpango wa ulinzi kwa mashahidi;
  5. Kusimamia maandalizi ya miongozo inayohusiana na uendeshaji wa kesi za jinai na utekelezaji wa maelekezo ya jumla ya upelelezi;
  6. Kusimamia utekelezaji wa maagizo yanayotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka kuhusiana na upelelezi wa kesi za jinai ili kuleta ufanisi;
  7. Kusimamia uratibu wa upelelezi ili kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwa na   mwendesha mashtaka;.
  8. Kusimamia na kufanya kaguzi katika maeneo ambayo mahabusu wanahifadhiwa na kuchukua hatua stahiki;
  9. Kufanya kazi na wadau wengine wa Haki Jinai ili kuwezesha uratibu wa kesi na ubadilishanaji wa taarifa; na
  10. Kuanzisha na kutunza mahusiano kati ya Ofisi, vyombo chunguzi na ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.

Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na Sehemu mbili (2) zifuatazo:

  1. Sehemu ya usimamizi wa kesi; na
  2. Sehemu ya uratibu wa upelelezi.

OFISI YA MASHTAKA YA MKOA

Lengo:  kutoa huduma za mashtaka Kwa umma katika ngazi ya mkoa

Majukumu:

Majukumu ya Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa ni haya yafuatayo:

  1. Kutoa huduma za kimashtaka mkoani ikiwa ni pamoja na kufungua, kuendesha au kuondoa mashtaka yaliyofunguliwa kwa minajili ya kutenda haki, maslahi ya umma na kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria.
  2. Kuratibu upelelezi na kutoa muongozo kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenye makosa ya udanganyifu, rushwa na   mengine yanayohusiana nayo;
  3. Kuandaa hati za mashtaka, maombi na nyaraka nyingine zinazoendeana na haya;
  4. Kusimamia kesi za rushwa zinazoshughulikiwa na mamlaka nyingine zinazopambana na rushwa na udanganyifu;
  5. Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi;
  6. Kutoa ushauri kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenye   makosa dhidi ya binadamu na mamlaka za umma;
  7. Kushughulikia kesi za   vifo vya mashaka;
  8. Kushughulikia   kesi za rufaa na maombi katika mahakama za juu;
  9. Kushughulikia mashahidi kabla, wakati wa kusikiliza kesi na baada ya kutoa ushahidi mahakamani;
  10. Kusimamia kesi zinazohusu makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu na madawa ya kulevya   ndani ya mamlaka yao;
  11. Kutoa mwongozo, kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika uhalifu na mazalia yake;
  12. Kuratibu kwa kushirikiana na wadau wa haki jinai kurejesha na kutaifisha mali haramu ndani ya mamlaka yao;
  13. Kuunganisha ofisi ya mashtaka na taasisi nyingine zinazoendesha mashtaka mkoani kwa lengo la kuhakikisha ufanisi katika upepelezi unaoratibiwa na mwendesha mashtaka;
  14. Kufanya ukaguzi sero za polisi na magereza;
  15. Kuwezesha kamati za usimamizi wa uendeshaji kesi katika ngazi ya mkoa na wilaya na majukwaa mengine;
  16. Kuandaa na kuchambua data za kesi za jinai;
  17. Kutunza kanzi data na mfumo wa taarifa wa mashtaka;  
  18. Kuelimisha umma kuhusu utenganiishaji wa upelelezi na uendeshaji wa mashtaka;
  19. Kutekeleza na kusimamia kanuni za nidhamu za waendesha mashtaka;
  20. Kuratibu uchukuaji wa waendeshaji wa mashtaka toka taasisi chunguzi mkoani;
  21. Kuanzisha na kutunza taarifa za waendesha mashtaka wote mkoani;
  22. Kuratibu na kuongoza taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya mazingira, kimtandao na makosa mengine yanayoendana na hayo;
  23. Kusimamia kesi za kimazingira na kimtandao zinazoendeshwa na mamlaka nyingine;
  24. Kushughulikia maswala ya kiutawala, kifedha na   kiutumishi katika mamlaka yao;
  25. Kufanya utafiti katika uendeshaji wa kesi za jinai ili kuhakikisha sharia, kanuni ,amri, taratibu na miongozo yote iliyokwishatolewa inafuatwa; na
  26. Kukagua na kufatilia uendeshaji wa kesi katika ofisi za mashtaka za wilaya ili kuhakikisha unafanyika kwa ufanisi. 

Ofisi za mashtaka za mikoa zitaongozwa na Afisa wa Mashtaka wa Mkoa.

OFISI YA MASHTAKA YA WILAYA

Lengo: kutoa huduma za mashtaka kwa umma katika ngazi ya wilaya

Majukumu:

Majukumu ya Ofisi ya Mashtaka ya Wilaya ni haya yafuatayo:

  1. Kutoa huduma za   kimashtaka wilayani ikiwa ni pamoja na kufungua, kuendesha  au kuondoa mashtaka yaliyofunguliwa kwa minajili ya kutenda haki, maslahi ya umma na kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria;
  2. Kuratibu upelelezi na kutoa muongozo kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenye makosa ya udanganyifu, rushwa na   mengine yanayohusiana nayo;
  3. Kuandaa hati za mashtaka, maombi na nyaraka nyingine zinazoendeana na haya;
  4. Kusimamia kesi za rushwa zinazoshughulikiwa na mamlaka   nyingine zinazopambana na rushwa na udanganyifu;
  5. Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi;
  6. Kutoa ushauri kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenye   makosa dhidi ya binadamu na mamlaka za umma;
  7. Kushughulikia kesi za   vifo vya mashaka;
  8. Kushughulikia   kesi za rufaa na maombi katika mahakama za juu;
  9. Kushughulikia mashahidi kabla, wakati wa kusikiliza kesi na baada ya kutoa ushahidi mahakamani;
  10. Kusimamia kesi zinazohusu makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu na madawa ya kulevya, ndani ya mamlaka yao;
  11. Kutoa mwongozo, kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika uhalifu na mazalia yake;
  12. Kuratibu kwa kushirikiana na wadau wa haki jinai, kurejesha na kutaifisha mali haramu ndani ya mamlaka yao;
  13. Kuunganisha ofisi ya mashtaka na taasisi nyingine zinazoendesha mashtaka wilayani kwa lengo la kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwa na mwendesha mashtaka;
  14. Kufanya ukaguzi sero za polisi na magereza;
  15. Kuwezesha kamati za usimamizi wa uendeshaji kesi katika ngazi ya wilaya na majukwaa mengine;
  16. Kuandaa na kuchambua data za kesi za jinai;
  17. Kutunza kanzi data na mfumo wa taarifa wa mashtaka; 
  18. Kuelimisha umma kuhusu   uchukuaji na uendeshaji wa mashtaka;
  19. Kutekeleza na kusimamia kanuni za nidhamu za waendesha mashtaka
  20. Kuratibu uchukuaji wa waendeshaji wa mashtaka toka taasisi chunguzi wilayani;
  21. Kuanzisha na kutunza taarifa za waendesha mashtaka wote wilayani;
  22. Kuratibu na kuongoza taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya mazingira, kimtandao na makosa mengine yanayoendana na hayo;
  23. Kusimamia kesi za kimazingira na kimtandao zinazoendeshwa na mamlaka nyingine;
  24. Kushughulikia maswala ya kiutawala, kifedha na   kiutumishi katika mamlaka yao; na
  25. Kufanya utafiti katika masuala ya jinai na uendeshaji wa kesi zake ili kuhakikisha sheria, kanuni, amri, taratibu na miongozo yote iliyokwishatolewa inafuatwa.

Ofisi ya Mashtaka ya Wilaya, itaongozwa na Afisa Mashtaka wa Wilaya

KITENGO CHA HUDUMA ZA UTAFITI NA MAKTABA

Lengo: kutoa utaalamu na huduma katika utafiti wa kisheria, huduma za uchapishaji na maktaba.

Majukumu:

Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:

  1. Kufanya utafiti wa kisheria katika uendeshaji wa mashtaka na masuala yanayohusiana nayo;
  2. Kuwajulisha watumiaji wa maktaba kuhusu bidhaa mpya za sheria;
  3. Kuwekea maktaba vifaa vya kutosha vya utafiti, nyenzo na nyaraka za rejea;