Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

UNICEF Support to Multisectoral

Mradi wa UNICEF Support to Multisectoral

Mradi huu unalenga kufanikisha Mipango ya Serikali inayohusu ulinzi na maendeleo ya mtoto nchini. Mradi huu umejikita katika kuimarisha utekelezaji wa mkakati wa pili wa taifa wa Haki Mtoto na usajili wa matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu, hususan usajili wa vizazi kwa watoto. Matokeo ya awali ya mradi huu ni usajili wa Watoto walio chini ya miaka mitano inafanyika mikoa na Wilaya zote za Tanzania Bara na ulinzi na upatikanaji wa haki za Watoto unaimarika. Matokeo ya kati ya mradi huu ni kuwa na mifumo thabiti ya kuwezesha upatikanaji wa haki mtoto nchini. Matokeo ya muda mrefu wa mradi huu ni haki za mtoto zinapatikana kwa wakati kwa maslahi mapana ya taifa.