Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Malengo:
Kutoa huduma na utaalamu katika habari, mawasiliano na mazungumzo na umma na vyombo vya Habari.
kitengo hiki kitatekeleza shughuli zifuatazo:
- kuzalisha na kusambaza nyaraka kama vile vipeperushi, makala, jarida la kuhabarisha umma kuhusu sera, programu, shughuli na maboresho yanayofanywa na wizara.
- Kuratibu mikutano ya Wizara na waandishi wa Habari.
- kushiriki katika majadiliano na umma pamoja na vyombo vya habari kuhusu masuala yanayohusu wizara.
- Kukuza, sera, programu na shughuli za Wizara.
- kuratibu utayarishaji wa nyaraka za wizara kwa ajili ya warsha na makongamano.
- kuratibu utayarishaji na utengenezaji wa makala za wizara na magazeti.
- Kuhuisha taarifa za Wizara katika tovuti.
- Kushauri Idara, vitengo na taasisi za umma juu ya utengenezaji wa nyaraka mbalimbali.
Hiki kitengo kinaongozwa na Mkuu wa Kitengo ambaye ni Afisa Habari Mkuu