Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Idara ya Haki za Binadamu

Malengo:

Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya haki za binafamu

Idara hii itatekeleza shughuli zifuatazo:

 1. Kutunga sera za haki za binadamu.
 2. kufanya mapitio ya sheria za ndani ili kuhakikisha sheria zilizopo za kimataifa na kikanda kuhusu haki za binadamu zinafuatwa.
 3. Kuhakikisha kwamba serikali inafuata wajibu wa haki za binadamu.
 4. Kuwezesha maridhiano kwa vyombo vya kimataifa na kikanda kuhusu haki za binadamu.
 5. kusimamia maendeleo ya mfumo wa haki za binadamu.
 6. kusimamia mfumo wa sera za utekelezaji wa haki za binadamu.
 7. kuwasiliana na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili Mkuu kuhusu masuala yanayohusu ushauri na masuala ya haki za binadamu.
 8. kuchambua na kushauri juu ya ripoti tofauti zilizowasilishwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Watendaji wengine wasio wa Kiserikali kuhusu haki za binadamu katika maeneo yanayohusiana.
 9. kuratibu masuala yanayohusiana na upatikanaji wa taarifa.
 10. kuratibu utayarishaji na uwasilishaji wa ripoti ya nchi juu ya maeneo tofauti ya utekelezaji kwa wizara, idara na wakala.

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu mbili kama ifuatavyo:-

 1. Sehemu ya ripoti za haki za binadamu
 2. Sehemu ya Uchunguzi wa Utekelezaji

 

Sehemu ya ripoti za haki za binadamu

Sehemu hii itatekeleza shughuli zifuatazo:

 1. Kuandaa sera za haki za binadamu.
 2. kusambaza maoni ya mwisho kutoka kwa mikataba ya mashirika ya haki za binadamu
 3. kuandaa ripoti za kitaifa kwa ajili ya kuwasilishwa mbele ya vyombo vya haki za binadamu.
 4. kuwezesha uidhinishaji wa hati za kimataifa na kikanda kuhusu haki za binadamu.
 5. kuwasiliana na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili Mkuu kuhusu masuala yanayohusu ushauri na masuala ya haki za binadamu.
 6. kuandaa ripoti za nchi kuhusu haki za binadamu kwa mujibu wa mikataba ya kikanda na kimataifa

 

Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

 

Sehemu ya Uchunguzi wa Utekelezaji

Sehemu hii itatekeleza shughuli zifuatazo:

 1. kuhakikisha kwamba serikali inafuata haki za binadamu
 2. kusimamia maendeleo ya mfumo wa haki za binadamu
 3. kuanzisha na kuendeleza mfumo  wa kisera kwa ajili ya utekelezaji wa haki za binadamu.
 4. kuwasiliana na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili Mkuu kuhusu masuala yanayohusu ushauri na masuala ya haki za binadamu.
 5. kufanya mapitio ya sheria za ndani ili kuhakikisha sheria zilizopo za kimataifa na kikanda kuhusu haki za binadamu zinzfuatwa.
 6. kufuatilia masuala yanayohusiana na upatikanaji wa taarifa.
 7. kuhamasisha viongozi wa umma kuhusu masuala ya haki za binadamu.

Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.