Bonanza la Kukata na Shoka Larindima Viwanja vya Sabasaba Njombe
Bonanza la Kukata na Shoka Larindima Viwanja vya Sabasaba Njombe
Imewekwa: 24 May, 2024

Na Lusajo Mwakabuku – WKS Njombe
Bonanza kali la kukata na shoka limerindima leo katika viwanja vya Sabasaba Njombe mjini ambapo vijana wa Bodaboda wameminyana na vijana wa Bajaji huku Bajaji wakiibuka washindi kwa mikwaju ya penati ya 5 - 4 wakati huohuo Mashabiki wa Yanga wakipambana na mashabiki wa Simba huku mashabiki wa Simba wakiibuka na ushindi wa goli 2-1. Michezo hii ni shamra shamra za kuelekea uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign 26/05/2024 ambapo Mgeni Rasmi ni Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.