Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Kuadhimisha Miaka 62

Imewekwa: 10 May, 2024
Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Kuadhimisha Miaka 62

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Mhe. David Kihenzile leo tarehe 10 Mei, 2024 ofisi za Bunge Dodoma. Kikao hicho kilihusu maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 62 ya Chama hicho nchini Tanzania yatakayofanyika Mei 11, 2024 Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu.