Chana Ashiriki Maadhimisho ya Mashujaa wa Vita ya Kwanza ya Dunia
Chana Ashiriki Maadhimisho ya Mashujaa wa Vita ya Kwanza ya Dunia
Imewekwa: 13 Nov, 2023
Na Lusajo Mwakabuku - WKS DSM
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameshiriki Ibada ya maadhimisho ya siku ya Mashujaa waliopoteza maisha wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia iliyofanyika kwenye makaburi ya Jumuiya ya Madola Kijitonyama, tarehe 12 Novemba, 2023 Jijini Dar es salaam.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano baina ya Ubalozi wa Uingereza na Ubalozi wa Ujerumani Waziri Chana amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuhamasisha Jamii na Nchi mbalimbali kuitunza na kudumisha amani.
Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Duniani hufanyika kila Jumapili ya kwanza baada ya Novemba 12 kila mwaka kwa lengo la kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha kwenye Vita ya Kwanza ya Dunia.