Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Dkt. Chana Ashiriki Mkutano wa Tanzania – Russia Alumni

Imewekwa: 08 Nov, 2023
Dkt. Chana Ashiriki Mkutano wa Tanzania – Russia Alumni

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt.  Pindi Chana ameshiriki Mkutano wa Wanafunzi waliohitimu Vyuo vikuu vya Nchini Urusi uliofanyika November 08, 2023 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Mhe. Chana ameipongeza Urusi kwa kuendeleza ushirikiano mzuri na Vyuo vya Tanzania katika kuboresha elimu na kuwakaribisha zaidi kuwekeza Tanzania kwani ni sehemu salama.

Aidha, kwa upande wake Balozi wa Urusi Nchini Andrey Avetsyan amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kwenda kusoma Nchini Urusi ili kudumisha ushirikiano kati Tanzania na Urusi kwa kubadilishana ujuzi katika tasnia mbalimbali.