Dkt. Chana Atembelea Chuo cha Uanasheria kwa Vitendo
Dkt. Chana Atembelea Chuo cha Uanasheria kwa Vitendo
Imewekwa: 18 May, 2024

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana leo Mei 18, 2024 Jijini Dar es Salaaam amefanya kikao na Uongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania) ukiongozwa Prof. Sist J. Mramba Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo ili kujadili kanuni na taratibu mbalimbali za uendeshaji Taasisi na kuona namna ya kuboresha kanuni hizo ili kukuza ufanisi katika mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo.