Dkt. Gwajima Aongoza Mkutano wa Jukwaa la Haki Jinai Kamati ya Mawaziri
Dkt. Gwajima Aongoza Mkutano wa Jukwaa la Haki Jinai Kamati ya Mawaziri
Imewekwa: 27 Jun, 2024

William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameongoza Mkutano wa Jukwaa la Haki Jinai Kamati ya Mawaziri kwa leo kama Mwenyekiti wa kikao hicho kilichofanyika Juni 27, 2024 Kumbi za Bunge Jijini Dodoma.
Katika Mkutano huo uliotanguliwa na Kikao cha Makatibu Wakuu, pamoja na mambo mengine wamejadili utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai Nchini, Taarifa ya Jukwaa la Haki Jinai Taifa na Taarifa ya ziara ya Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipotembelea baadhi ya Magereza Nchini.