Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Dkt. Ndumbaro apokea Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria

Imewekwa: 11 Apr, 2023
Dkt. Ndumbaro apokea Taarifa ya Mapitio ya Mfumo wa Sheria

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amepokea Taarifa za mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia Uchaguzi na Vyama vya Siasa Nchini na Mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia utoaji haki katika Mahakama za Mwanzo kutoka kwa Mhe. January H. Msoffe (Jaji Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, tarehe 11 Aprili, 2023 Ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma. Taarifa hizo zitawasilishwa Bungeni kwa mujibu wa sheria ili mchakato wa mabadiliko ya sheria hizo uanze.

Katika hafla hiyo Dkt. Ndumbaro ametoa rai kwa Wizara na Taasisi zote za umma zinazotaka kufanya tafiti, marejeo au uboreshaji wa sheria zao kutumia Tume ya Kurekebisha Sheria kwani ndiyo yenye mamlaka kufanya kazi hiyo.