Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Dkt. Ndumbaro Aongoza Kikao cha Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.

Imewekwa: 11 Aug, 2023
Dkt. Ndumbaro Aongoza Kikao cha Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameongoza Kikao Kazi cha kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali yenye lengo la kuboresha mifumo ya utoaji huduma, utekelezaji wa majukumu na kutoa mikanganyiko ya kisheria katika utendaji kwenye Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Katika Kikao Kazi hicho kilichofanyika kwenye Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023 na kuhudhuriwa na Menejimenti ya Wizara na kuwashirikisha Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, miswada ishirini na tatu ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria iliwasilishwa na kujadiliwa. Mhe. Ndumbaro pamoja na mambo mengine alisisitiza tafiti za kisayansi kuendelea kufanyika kabla ya mapendekezo yoyote ya mabadiliko ya sheria. 

Mapendekezo ya kurekebisha ya sheria hizo yaliwasilishwa na Bw. Abdulrahman Mshamu Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma.