Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Gekul awataka waajiriwa wapya kuepuka vitendo vya ukiukaji wa maadili ya kazi

Imewekwa: 24 Mar, 2023
Gekul awataka waajiriwa wapya kuepuka vitendo vya ukiukaji wa maadili ya kazi

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amewataka waajiriwa wapya kuwa na uweledi, kuepuka vitendo vya ukiukaji wa maadili ya kazi pamoja na kuepuka rushwa, uonevu na matumizi mabaya ya ajira zao.

Mhe. Gekul aliyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, yaliyofanyika Mkoani Morogoro, Hoteli ya Kingsway kuanzia tarehe 17-23 Machi, 2023.