Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Huduma ya Msaada wa Kisheria kuwa Endelevu.

Imewekwa: 03 Aug, 2023
Huduma ya Msaada wa Kisheria kuwa Endelevu.

Na Felix Chakila - WKS Dar es Salaam

Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mtandao wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria (TANLAP) na Menejimenti ya Legal Services Facility “LSF” tarehe 03 Agosti, 2023 jijini Dar es Salaam na kujadili masuala ya msaada wa kisheria na ufahamu wa masuala ya sheria ili kuona namna ya kuwa huduma ya msaada wa kisheri inavyokua endelevu nchini.

“Ni vyema mara baada ya kutekeleza Kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Sheria katika mkoa husika kukawa jitihada za kuifanya Kampeni kuwa endelevu ili wanachi waendelee kupata huduma. Niwasihi TANLAP na wadau wengine wakiwemo Chama cha Wanasheria Tanganyika kutumia Ofisi ambazo zipo katika maeneo husika na kuwezesha migogoro iliyoibuka iweze kushughulikiwa.” Alisema Dkt. Ndumbaro.

Katika mazungumzo hayo, Uongozi wa TANLAP umewasilisha ombi kwa Serikali kuendelea kuangalia kwa jicho la ukaribu Sheria zinazohusu ndoa na mirathi kwa kuwa zimekua zikiongezeka kwa kiwango kikubwa na pia ipo haja ya Serikali kuongeza rasilimali watu katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Temeke kinachoshughulikia migogoro ya Mirathi na Ndoa.