Kabudi Aongoza Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa AALCO Thailand
Kabudi Aongoza Ujumbe wa Tanzania Mkutano wa AALCO Thailand
Imewekwa: 11 Sep, 2024
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba J. A. Kabudi, Septemba 11, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Polcol Tawee Sodsong, Waziri wa Sheria wa Thailand ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia maeneo ya ushirikiano hususan kuwa na programu za mafunzo na kubadilishana uzoefu katika masuala ya sheria za uwekezaji na sekta ya sheria kwa ujumla.
Waziri Kabudi anaongoza ujumbe kutoka Tanzania nchini Thailand unaoshiriki Mkutano Mkuu wa 62 wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria wa Kimataifa wa Nchi za Asia na Afrika (AALCO).