Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Kampeni ya Msaada wa Kisheria Kufanyika Mikoa Minne kwa Pamoja

Imewekwa: 18 Oct, 2024
Kampeni  ya Msaada wa Kisheria Kufanyika Mikoa Minne kwa Pamoja

Wizara ya Katiba na Sheria ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kuendeleza utekelezaji wa kampeni ya msaada wa kisheria katika Mikoa Minne ambayo ni Mororgoro, Iringa, Songwe na Mara.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi wakati akimwakilisha Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria katika kufungua mafunzo ya siku tatu kwa wataalam kutoka taasisi mbalimbali za kisheria ambao ndio watakuwa viongozi wa timu zitakazotoa huduma ya Msaada wa Kisheria katika mikoa tajwa.