Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Yaanza Viwanja vya Nyerere Dodoma

Imewekwa: 24 Jan, 2024
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Yaanza Viwanja vya Nyerere Dodoma

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Madhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo huandaliwa na Mahakama ya Tanzania kila mwaka yameanza leo tarehe 24 Januari, 2024 kwenye viwanja vya Nyerere Square, Jijini Dodoma ambapo Wizara ya Katiba na Sheria inashiriki.

Maadhimisho hayo ya siku tisa yaliyobeba kauli mbiu ”Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai” yatazinduliwa rasmi tarehe 27 Januari, 2024 na kufungwa rasmi tarehe 1 Februari, 2024. Wakati wote wa maadhimisho hayo Wizara itakuwa inatoa elimu ya sheria na huduma ya msaada wa kisheria.