MASWI AIPONGEZA RITA KWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi amepongeza utendaji kazi wa Wakala wa Usajili ufilisi na Udhamini (RITA) kwa huduma wanazotoa kwa wananchi na kusifu huduma kwa njia ya Kidigitali ilivyorahisisha ufanyaji maombi ukiwa popote.
Maswi ameyasema hayo mapema hii leo Agosti 10, 2025 aliposhiriki katika maadhimisho ya siku ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu barani Afrika (CRVS DAY) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nanenane Jijini Dodoma ambapo pia alipata fursa ya kutembelea banda la Wakala kuona namna huduma mbali mbali zinavyotolewa.
Aidha Kabidhi wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili na Ufilisi na Udhamini (RITA) Bw. Frank Kanyusi amesema kuwa RITA inaendelea kujikita kidigitali kwa kuelekea kuwa na huduma ya e-certificate ambayo itakuwa inamuwezesha mwananchi kupata nakala yake ya cheti bila kufika ofisini.
Wakala umeendelea kuadhimisha siku hiyo muhimu ikiwa ni maadhimisho ya nane huku ukitoa huduma za kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa wananchi.